Psalms 72

Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme

(Zaburi Ya Sulemani)


1 aEe Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,
mwana wa mfalme kwa haki yako.

2 bAtawaamua watu wako kwa haki,
watu wako walioonewa kwa haki.

3 Milima italeta mafanikio kwa watu,
vilima tunda la haki.

4 cAtawatetea walioonewa miongoni mwa watu
na atawaokoa watoto wa wahitaji,
ataponda mdhalimu.

5 dAtadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

6 eAtakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,
kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

7 fKatika siku zake wenye haki watastawi;
mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.


8 gAtatawala kutoka bahari hadi bahari
na kutoka Mto
Yaani Mto Frati.
mpaka miisho ya dunia.

9 Makabila ya jangwani watamsujudia,
na adui zake wataramba mavumbi.

10 iWafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.

11 jWafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.


12 Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,
aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.

13 kAtawahurumia wanyonge na wahitaji
na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.

14 lAtawaokoa kutoka uonevu na ukatili,
kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.


15 mAishi maisha marefu!
Na apewe dhahabu ya Sheba.
Watu wamwombee daima
na kumbariki mchana kutwa.

16 nNafaka ijae tele katika nchi yote,
juu ya vilele vya vilima na istawi.
Tunda lake na listawi kama Lebanoni,
listawi kama majani ya kondeni.

17 oJina lake na lidumu milele,
na lidumu kama jua.

Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,
nao watamwita aliyebarikiwa.


18 p Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,
yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.

19 qJina lake tukufu lisifiwe milele,
ulimwengu wote ujae utukufu wake.
Amen na Amen.

20 rHuu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.
Copyright information for SwhKC